April 19, 2018





Mabingwa wa soka wa Tanzania, Yanga wanatarajia kuwasili kesho saa 7 alfajiri.

Yanga imefanikiwa kuingia katika hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho baada ya kufungwa kwa bao 1-0. Wamevuka kwa jumla ya mabao 2-1 baada ya ushindi wa 2-0 jijini Dar es Salaam.

Maana yake ni usiku wa kuamkia leo na mashabiki wametakiwa kujitokeza kwa wingi kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Katibu Mkuu wa Yanga, Charles Boniface Mkwasa amesema kikosi chao kinawasili na tayari wametoa wito huo.

“Tumetoa wito kwa mashabiki kujitokeza kwa wingi na kuipokea timu. Inawasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere kutumia ndege ya Shirika la Ndege la Kenya,” alisema.

Mkwasa alisema baada ya kikosi chake kurejea wataendelea na maandalizi ya Ligi Kuu Bara.





0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic