Kocha wa Dodoma FC, Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ amefunguka kuwa kuondoka kwa Mzambia George Lwandamina aliyekuwa kocha mkuu wa timu hiyo, ni pigo na huenda ikawaathiri wachezaji kisaikolojia kutokana na michuano iliyopo mbele yao.
Hivi karibuni, Lwandamina aliondoka Yanga na kwenda kuingia mkataba na klabu ya nchini kwao, Zesco United ambayo alikuwa akiifundisha kabla ya kutua hapa nchini.
Julio alisema kuwa kuondoka kwa kocha huyo ni pigo kwa Yanga hasa kutokana na hali ambayo inapitia timu hiyo kwa sasa.
Julio alisema kuondoka kwa Lwandamina huenda kukawaathiri wachezaji kisaikolojia na bado wakiwa na majukumu mazito mbele yao.
“Yanga ni timu inayopambana msimu huu lakini kitendo cha Kocha Lwandamina kuondoka na timu ikiwa inamhitaji ni pigo sababu wana michuano mikubwa mbele yao.
“Lakini hawapaswi kukata tamaa sababu mimi ninamuamini (Shadrack) Nsajigwa ni kocha mzuri ambaye tayari amekaa na makocha hao wakubwa wenye uzoefu, hivyo anaweza kupambana na kuweza kuibeba Yanga,” alisema Julio.
SOURCE: CHAMPIONI
Nsajigwa hawezi kuwafanya wachezaji warudi kwenye hali yao...bado technique si mzoefu..siwezi kumpa nafasi kubwa..sana tutapotea kabisa. Hapa inatakiwa itafutwe njia mbadala. Naamini Yanga ikipita round hii kwenye kimataifa inategemea kupewa kama milioni mia sita hivi. Wachezaji wajitahidi. Maana kwa wastani wakichukua hiyo hela na kila mchezaji akilipwa pesa yake kwa wastani wa milioni tatu kwa mchezaji itakuwa imetumika milioni 180 kwa miezi mitatu. Zitabaki akiba ya 420m. Wachezaji wajengewe ushupavu wa kupambana. Mkwasa achukue hilo jukumu la muda asaidiane na Nsaigwa. Etiene hana sifa za kuifundisha Yanga bhana..lazima tuangalie kocha mwenye msaada mkubwa kwetu
ReplyDelete