April 15, 2018






MUNICH, Ujerumani
KLABU ya Bayern Munich ndiyo pekee kubwa ambayo ndani ya eneo la uwanja wake, kuna msikiti.

Klabu maarufu ya FC Barcelona ya Hispania, wao ndani kabisa ya uwanja kuna kanisa ambalo hutumiwa zaidi na wachezaji na baadhi ya viongozi.



Lakini Bayern wameamua kujenga msikiti katika eneo la ndani ya uwanja wake na zilipo ofisi za makao makuu ya klabu hiyo tajiri na maarufu zaidi nchini Ujerumani.

Bayern ni moja ya klabu kubwa zaidi barani Ulaya na imewashangaza wengi baada ya kusikiliza wazo la kiungo wake mkongwe, Frank Ribery ambaye aliushauri uongozi kujenga angalau msikiti mdogo.


Baadaye uongozi wa Bayern ulilifanyia kazi suala hilo na kuujenga msikiti huo maarufu kwa jina la Masjid Canggih di Markas ukiwa ndani ya eneo ulipo Uwanja wa Allianz Arena kwenye upande uliopewa jina la Cologne Central Mosque.

Waislamu wanaruhusiwa kuutumia msikiti wakati wowote na kitu kizuri zaidi, klabu inauendesha kwa kutoa fedha kwa asilimia 85 huku asilimia 15 iliyobaki inatolewa na wachezaji Waislamu wanaoichezea Bayern.

Unaweza kudhani ni msikiti mdogo, kwani hata wakati Ribery akitoa wazo, aliwaeleza msikiti mdogo wa saizi ya kati. Lakini Bayern hawakutaka kubahatisha katika hilo baada ya kujenga msikiti wenye uwezo wa kubeba watu 1,200.

Kwa kiasi fulani, msikiti huo haujawa maarufu sana kwa kuwa vyombo vingi vya habari vya Ulaya havikuona kama ni jambo la kulitangaza sana au waliona ni jambo la kawaida tu.


Kivutio zaidi, msikiti huo umekuwa maarufu zaidi barani Asia ambako kuna Waislamu wengi zaidi na wengi wanaotembelea eneo hilo wamekuwa wakijitokeza kwa wingi kuutembelea au kwenda kusali.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic