April 12, 2018



Na George Mganga

Mtibwa Sugar imefanikiwa kuibuka na ushindi kiduchu wa bao 1-0 dhidi ya Ndanda FC katika mchezo wa Ligi Kuu Bara uliopigwa Uwanja wa Manungu leo.

Kikosi hicho kimejipatia bao lake kupitia kwa Kelvin Sabato aliyefunga katika dakika ya 22 ya kipindi cha kwanza.

Wakata miwa hao wa Morogoro wamepata matokeo baada ya kupoteza mechi iliyopita dhidi ya Simba kwa kichapo cha bao 1-0.

Mtibwa sasa imefikisha jumla ya alama 33 kwenye msimamo wa ligi huku ikicheza michezo 23 na ikiwa nafasi ya 6.

Wakati huo Ndanda FC imekamata nafasi ya 12 ikijikusanyia alama 23 huku ikicheza jumla ya mechi 24 msimu huu.

Mechi nyingine ambayo ilipaswa kupigwa Uwanja wa Mabatini leo ilikuwa ni kati ya Ruvu Shooting FC dhidi ya Azam FC. 

Mtanange huo umeahirishwa kutokana na mvua kubwa kunyesha huku ikisababisha Uwanja wa Mabatini kujaa maji.

1 COMMENTS:

  1. Leo pale Taifa hajafungwa mbeya city pekee,kafungwa yanga,azam,singida na mtibwa na bado tunaendelea kugawa dozi.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic