April 19, 2018


Hatimaye Nyota wa Bongo Fleva, Ali Saleh Kiba ‘King Kiba’, amefunga ndoa na mchumba wake Amina Khalef, leo asubuhi, Aprili 19, mjini Mombasa nchini Kenya.

Hakika ni furaha, shangwe, nderemo na vifijo kwa maharusi, wanafamilia na mashabiki wa Kiba mara baada ya ndoa hiyo kufungwa katika msikiti wa Ummul Kulthum, mjini Mombasa.




Ilikuwa ni baada Koran kusomwa, na Sheikh Mohammed Kagera akakinyanyua kiganja cha Alikiba na kumuozesha kwa Amina Khalef.

“Mimi Ali Saleh nimekubali kumuoa Amina Khalef kwa mahari tuliyokubaliana na ikitokea sababu ya kuachana tuachane kwa wema,” amesema Kiba wakati akifunga ndoa yake.


Katika shughuli hiyo, Kiba alivaa joho na kilemba, alishika upanga kama desturi ya tamaduni ya zinavyomtaka na baada ya kutoka msikitini waalikwa wamekwenda nyumbani kwa ndugu wa Joho, Abu Joho, Kizingo.







Unaweza ukatazama video ya tukio hilo namna ilivyokuwa hapa



0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic