April 19, 2018



Kikosi cha simba kimewasili salama Iringa mjini jioni ya leo kwa ajili ya mchezo wa ligi dhidi ya Lipuli FC.

Simba ilikuwa mjini Morogoro kuweka kambi maalum ya siku moja kwa ajili ya maandalizi kuelekea mchezo huo.

Baada ya kuwasili mjini humo, Simba itafanya mazoezi yake ya mwisho kesho kwenye Uwanja wa Samora, kabla ya kuvaana na Lipuli Jumamosi ya wiki hii.

Taarifa zinaeleza kuwa hali ya wachezaji wa kikosi hicho kwa ujumla iko vizuri na morali ipo kuelekea mechi hiyo.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic