April 2, 2018



Kikosi cha timu ya taifa ya wanawake kutoka Zambia kimewasili mchana huu jijini Dar es Salaam tayari kwa ajili ya mchezo wa kuwania kufuzu Kombe la Mataifa ya Afrika kwa wanawake dhidi ya twiga Stars.

Zambia maarufu kama 'Shepolopolo' wametua mchana wa leo Uwanja wa Kimataifa wa Julius Kambarage Nyerere na kupokelewa na baadhi ya viongozi wa TFF.

Kikosi hicho cha Zambia kitacheza na Twiga Jumatano ya wiki hii katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Baada ya mechi hiyo kumalizika, mchezo wa marudiano utafanyika baada ya wiki mbili nchini Zambia.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic