April 19, 2018



Mshambuliaji wa zamani wa Simba na Yanga, Hamis Kiiza, ametoa utabiri wake kuelekea mechi ya watani wa jadi kati ya Simba na Yanga itakayopigwa Uwanja wa Taifa, Aprili 29 2018.

Kiiza ameeleza mechi hiyo itakuwa ngumu kutokana na namna asili ya timu hizo ilivyo kwa kusema yeyote atakayejipanga vizuri atapata matokeo.

Mchezaji huyo aliyeweza kung'ara wakati anazichezea klabu hizo kongwe za Kariakoo, ameweka utabiri wa asilimia 50 kwa 50 akidai mara nyingi mtanange huo huwa hautabiriki.

Kiiza hivi sasa yuko zake Ethiopia akisakata kabumbu baada ya kutoka Tanzania na baadaye kutimkia Uganda, kabla ya kuelekea Ethiopia.

Simba itakuwa mwenyeji wa pambano hilo litakalopigwa Uwanja wa Taifa, ambapo katika mechi ya mzunguko wa kwanza wa ligi, timu hizo zilenda sare ya 1-1.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic