April 6, 2018



Na George Mganga

Afisa Habari wa klabu ya Yanga, Dismas Ten, amemjibu Haji Manara juu ya kile alichokiandika kupitia ukurasa wake wa Instagram akilikejeli tangazo la timu hiyo linalowataka mashabiki wa Yanga kujitokeza Uwanjani kesho.

Yanga waliweka tangazo linaloonesha picha za akina dada waliovaa jezi la rangi ya njano likieleza kuwataka mashabiki wa timu hiyo wajitokeze wakiwa wamevalia uzi wa njano kuisapoti ikicheza dhidi ya Welayta Dicha FC katika mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika.

Baada ya Afisa Habari wa Simba, Manara kuliona tangazo hilo aliandika ujumbe kupitia Instagram akieleza kuwa akina dada hao ni wanene na hawana maumbile mazuri kutumika kwenye tangazo hilo huku akiwaita mitulinga.

Kufuatia Manara kuandika hivyo, Ten amemjibu Manara kwa kumweleza kuwa akina dada hao ndiyo waliomchangia wakati anaumwa macho na kumfanya apelekwe hospitalini kufanyiwa matibabu.


"Asante ndugu yangu kwa 'kunitag' Ila naomba nikukumbushe tu, akina dada hao unaowaita 'Mitulinga' Leo.! Ndiyo waliotoa hela (tena waliyoitafuta kwa jasho lao) kukuchangia ukapate matibabu nauliipokea, dunia iliona. Hakika tunapaswa kumshukuru Mungu kwa kila jambo" aliandika Ten.



5 COMMENTS:

  1. Inawezekana majibu ya msemaji wa Yanga Ditmass Ten yakawa na uhalisia kuwa Khaji Manara alipata msaada kutoka kwa aina ya kina dada waliogandishwa pichani katika tangazo la Yanga lakini ni ukweli usiopingika hata kidogo kuwa majibu ya Dismas ameyajenga katika misingi ya kisiasa zaidi na kwa upande mwengine tunweza kusema ni masimango kwani unapomsaidia mtu kwa nia ya kweli na kiroho basi hata pakitokea tofauti kati yenu huna haja ya kukumbusha masuala ya misaada ya kibinaadamu uliotoa. Khaji Manara licha ya kudaiwa kutoa kejeli kwa maumbile boga au miili maji kwa wale wadada wa tangazo la Yanga lakini kiukweli na bila ya kumumunya maneno Manara yupo sahihi kabisa. Unene ni maradhi sio urembo athlani. Watanzania tuachane na kasumba yakuwa unene ni kitu cha kuwaringishia watu wengine Dunia inatucheka kwa ujinga wetu. Kuna unene wa afya ambao mtu akiwa nao hata kipofu atasifu kuwa mwanadada kukatika sihaba. Lean body mass,ujazo wa mwili uliogangamala na haiba ya mtu na sio,Fat sagging body mass ambayo ni aina ya miili watanzania wengi tumekuwa tukiishi nao na kujivunia na si kwa wanawake si wanaume bila yakujua kuwa tabia hiyo ya kuendekeza miili minene ni sawa na mtu alieamua kumeza bomu lilowekewa timer na kuamua kuendelea na shughuli zake kana kwamba hakuna kinachoendelea mwilini mwake na mwisho ya siku vijana wadogo wanakatishwa maisha yao kwa matatizo ya blood pressure,kisukari, Matatizo ya macho, Matatizo ya uzazi,figo,ufanisi duni na wa aibu katika tendo la ndoa nakadhalika nakadhalika. Kwa wenzetu nchi zilizoendelea unene ni janga la taifa. Na mara nyingi unene huusishwa na watu wenye elimu duni na mara nyingi watu wa kipato cha chini. Vile uvivu ni moja ya sababu moja kubwa hasa katika suala la mazoezi. Kwa kwetu Tz hapana shaka unene ni kwa watu wenye kipato kizuri kwa hivyo utaona tuna tatizo la elimu ya lishe kwa watanzania. Kwa nchi zilzoendelea tatizo la unene limefungua fursa mpya za ajira kama vile vituo na vifaa vya mazoezi na hata bidhaa za vyakula vinaharakisha kuurejesha mwili katika mtizamiko wa hali yake ya afya . Watanzania tunatakiwa kubadilika na tuache siasa za kijinga na kwa hili Manara yupo sahihi kabisa licha yawesekana uwasilishaji wa ujumbe wake haukuwapendezesha baadhi ya watu. Na kwa maoni yangu mwenye kununa muache anune lakini ukweli ni TIBA kuliko sindano.

    ReplyDelete
  2. Maneno ya Haji Manala kwa akina Dada wa liomo kwenye tangazo LA Yanga in unyanyasaji,na kunyapalisha.hayakubaliki kisheria katika ulimwengu was mpira duniani.Makosa kumdhihaki mwingine kwa kutazama rangi ya MTU na maumbile yake.hill lisiangaliwe kiushabiki.Wanaomtetea Manara wajue maneno ya Manara yangesemwa na wengine kwake kwa kuangalia maumbile Manala asingekamatika.huo no ukorofi was kijinai.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Dis Ten yuko sahihi Haji hauko sawa ukinyooshewa kidole ww kwa mtindo huo huo dunia haitakubali jitafakari saana kabla ya kuchokoza wengine.

      Delete
    2. Dis Ten yuko sahihi Haji hauko sawa ukinyooshewa kidole ww kwa mtindo huo huo dunia haitakubali jitafakari saana kabla ya kuchokoza wengine.

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic