April 6, 2018




Uongozi wa Singida United licha ya kupokea kichapo cha mabao 3-0 kutoka kwa Mtibwa Sugar jioni ya leo, umeibuka na kusema timu kubwa imefungwa magoli mepesi.

Akizungumza kupitia kipindi cha E Sports ya EFM jioni ya leo, Mkurugenzi wa Singida United, Festo Sanga, amesema wamekubali matokeo huku akieleza wamefungwa magoli mepesi leo.

Sanga amekubali matokeo hayo huku akikumbushia pia kuwa waliwahi kufungwa mabao 4-0 na Simba Uwanja wa Taifa hivyo wamedai kuchukulia kama sehemu ya mchezo.

Mtibwa imeibuka na ushindi huo ikiwa inasubiriwa na Simba mjini Morogoro katika mchezo mwingine wa Ligi, Jumatatu ya wiki ijayo.

Kipigo hicho kwa Singida kimekuja baada ya kuiondoa Yanga kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho kwa changamoto ya mikwaju ya penati (4-2).

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic