April 6, 2018




Msemaji wa klabu ya mtibwa Sugar, Thobias Kifaru, ameitambia Simba kuwa lazima waimalize katika mchezo ujao wa ligi utakaopigwa Jamhuri Stadium.

Kifaru ametamba kufuatia ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Singida United uliopigwa Uwanja wa Namfua mjini Singida leo.

Mtibwa itakuwa inacheza na Simba katika Uwanja wake wa nyumbani Jumatatu ya Aprili 9 2018 kuanzi saa 10 kamili jioni.

Tayari Simba walishawasili mjini Morogoro kwa ajili ya mchezo huo wakitokea Iringa leo ambapo waliweka kambi maalum kuendeleza mawindo dhidi ya wakata miwa hao.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic