April 1, 2018





Kocha George Lwandamina na Kipa Ramadhan Kabwili wako njiani hivi sasa kuelekea Singida kwa ajili ya kukiongezea nguvu kikosi cha Yanga.

Taarifa zinaelezwa kuwa Lwandamina alisafiri kuelekea Ethiopia kuwasoma wapinzani wake, Welayta Dicha, ambao atakutana nao katika Kombe la Shirikisho Africa.

Ramadhan Kabwili yeye alisalia jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kuitumikia timu ya taifa ya vijana, chini ya miaka 20 iliyokuwa ikimenyana na Congo katika mchezo wa kuwania nafasi ya kushiriki AFCON U20.

Yanga itakuwa mgeni wa Singida United katika mchezo wa Kombe la Shirikisho utakaopigwa majira ya saa 10 kamili jioni.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic