April 19, 2018




Airtel Tanzania imetajwa kuwa moja ya makampuni bora ambayo yanajibu vizuri maswali ya mashabiki na wateja wake katika robo mwaka ya kwanza ya mwaka 2018.

Ripoti hii imetolewa na kampuni ya Socialbakers ambayo ni moja ya makampuni yanayoongoza duniani katika kutoa tathmini kuhusu namna makampuni mbalimbali yanawajibika katika kujibu maswali ya wateja wao katika mitandao ya kijamii. 

Kwa mujibu wa Socialbakers, tathmini ya robo hii ya mwaka ilifanyika kuanzia Januari 1, 2018 hadi Machi 31, 2018 na kuifanya Airtel Tanzania iibuke kidedea.

Kampuni hiyo ya Social bakers imekabidhi cheti kama ishara ya ushindi huu na kuonesha kuwa Airtel iliweza kujibu vizuri maswali ya mashabiki wake na wateja kupitia mtandao wa Face book kwa asilimia 98 na hivi kuyapiku makampuni mengine yote ya simu Tanzania. 

Mkurugenzi wa Masoko wa Airtel Tanzania, Bwn Isack Nchunda alisema wanajivunia kupata utambulizi huo na inaonesha jinsi gani wamekuwa wakijituma kuhakikisha wateja wao wanapata majibu ya maswali yao kwa wakati kupitia mitandao ya kijamii hususani Face book. 

“Tunayo faraja kuweza kutambuliwa kwa namna hii na sisi tunalo jukumu la kuendelea kuhakikisha wateja na mashabiki wetu wanapata majibu wanayohitaji kwa wakati na mitandao ya kijamii imeturahisishia kazi hii hususani kupitia Face book tumeweza kujibu maswali kwa haraka na kwa wateja wengi zaidi kwa wakati mmoja,” alisema. 
Mitandao ya kijamii kama Face book inatakiwa kutangazwa zaidi ili itumike kwa wingi kwani itapunguza usumbufu wa wateja kusubiri majibu kwa muda mrefu kama ilivyokuwa hapo awali ambapo walilazimika kupiga simu Airtel. “Kwa kupitia mitandao ya kijamii majibu yanatolewa hapo hapo na hili ndilo limetufanya tutambuliwe kwani tumeweza kutumia njia hii kwa ufanisi mkubwa na tathmini ya Socialbakers imeonesha kuwa katika robo ya kwanza ya mwaka huu tulijibu maswali kwa asilimia 98 na hivi kuibuka kidedea,” aliongeza Ndunda
Kwa mujibu wa Socialbakers, utambulizi huu unatokana na namna kampuni imeweza kujibu maswali ya watu kwa muda wa mwezi mitatu. Ili utambuliwe, lazima kampuniipokee maswali 50 kutoka kwa mashabiki katika robo husika na maswali hayo yaweze kujibiwa kwa zaidi ya asilimia 65. 
Socialbakers ni moja ya makampuni yanayoongoza duniani katika kutoa tathmini kuhusu namna makampuni mbalimbali yanawajibika katika kujibu maswali ya wateja wao katika mitandao ya kijamii hususani Face book, Twitter, Google+, LinkedIn na YouTube ili kusaidia makampuni kujua mafanikio ya kampeni mbalimbali kupitia mitandao hii.  

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic