April 7, 2018



Na George Mganga

Hatua ya mkondo wa kwanza wa Kombe la Shirikisho Afrika unaanza leo ambapo Yanga itakuwa inacheza na Welayta Dicha FC kutoka Ethiopia kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Yanga inaenda kucheza mchezo huo ikiwa imetoka kuondolewa Ligi ya Mabingwa Barani Afrika dhidi ya Township Rollers FC kutoka Botswana kwa jumla ya mabao 2-1.

Mabingwa hao watetezi walipangwa kucheza na Waethiopia hao baada ya kufanyika kwa droo wiki kadhaa zilizopita na CAF

Kikosi hicho kitakuwa kinawakosa wachezaji kadhaa, Kelvin Yonda, Papy Kambamba, Said Makapu pamoja na Obrey Chirwa ambao kwa mujibu wa CAF imesema wanatumikia adhabu ya kuwa na kadi mbili za njano.

Mchezo huo utakoanza saa 10 kamili utaifanya Yanga ianze kuzisaka milioni 600 endapo itapata matokeo mazuri leo pamoja na katika mchezo wa marudiano, endapo itafanikiwa kuingia hatua ya makundi.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic