April 29, 2018




Mashabiki wa Yanga kutoka makundi mbambali ya WhatsApp, yamechangishana kukusanya kiasi cha shilingi milioni tatu na kuziwalisha kwa wa timu yao ili kutoa motisha.

Mashabiki hao wamefikia hatua ya kufanya hivyo ili kutoa hamasa kwa wachezaji ambao wana kibarua dhidi ya watani zao wa jadi Simba SC kwenye mchezo wa ligi kuu.

Fedha hizo zimewasilishwa kwa wachezaji hao na kiongozi wa makundi hayo, kisha kuzikabidhi mbele ya beki ya namba mbili, Juma Abdul aliyekuwa sambamba na Meneja wa Yanga, Hafidh Saleh.



Imekuwa ni utaratibu wa kawaida kwa mashabiki na wanacham wa timu hizo mbili za kariakoo, Simba na Yanga kujitoa kwa ajili ya timu zao kwa kuchangishana fedha ili kutia morali na hamasa kwa wachezaji.

1 COMMENTS:

  1. Naomba niunganishwe kwenye group moja ya Yanga Whatsapp kwa number hii tafadhali. Mimi ni shabiki wa Yanga damu. +18708164743

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic