BAADA YA KUELEZWA KUWA ATAKOSEKANA MICHUANO YA KOMBE LA DUNIA, SALAH AANDIKA UJUMBE HUU
Baada ya kuenea kwa taarifa zilizoeleza kuwa nyota wa Liverpool na timu ya Taifa ya Misri, Mohamed Salah atakosekana katika fainali za michuano ya Kombe la Dunia huko Russia, mchezaji huyo amesema atakuweko kwenye mashindano hayo.
Salah aliumia jana juzi katika mchezo wa fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya wakati Liverpool baada ya kuchezewa rafu na beki wa Real Madrid, Sergio Ramos katika mchezo ambao ulimalizika kwa Madrid kushinda mabao 3-1 na kunyakua ubingwa.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram na Twitter pia Facebook, Salah ameandika kuwa ana imani atakuwepo kwenye michuano ya Kombe la Dunia huko Urusi inayotaraji kuanza siku kadhaa zilizosalia.
Kauli hiyo inaonesha kuwa mchezaji huyo hajaumia vibaya hivyo kuna uwezekano mkubwa wa kuwa na kikosi cha timu ya taifa ya Misri kwenye michuano hiyo mikubwa duniani licha ya taarifa zilizoripotiwa awali kusema anaweza akakosekana.
Kufuatia rafu hiyo aliyochezewa na Ramos, Salah ilibidi aondolewe Uwanjani na nafasi yake kuchukuliwa na Adam Lallana katika dakika ya 30 ya kipindi cha kwanza na kufanya safu ya ushambuliaji ya Liverpool kupunguza makali na Madrid kuzidi kutawala zaidi.
KWANI UNAJUA MI ATA HUWA SIKUELEWAGI YANI, HAIWEZEKANI SALAH AUMIE MKONO ALAFU UTUWEKEE PICHA AMESHIKA MAGONGO, NI AINA GANI HII YA UANDISHI..ANAWEZAJE KUSHIKA MAGONGO ILALI ULIOUMIA NI MKONO, DUUUUH
ReplyDeleteHahahaaaa huyu Saleh Nanga kweli
DeleteYaan hyo picha sijui kaitoa wapi
Ni sawa na kuumia mkono alafu unafanyiwa operation ya kichwa 😄😄
Hhhhhhh, ... mi nilijua tu kuwa ile ilikuwa geresha. Liverpool walishajuwa kuwa ngoma ni nzito. Walishatambua mapema kabisa kuwa muziki ule ulikuwa ni mkubwa sana kwao, na kwamba wazingeuweza.
DeleteWakaamua kutumia mbinu hii ya kujiangusha hovyo hovyo ili wapate huruma ya marefa na pia wajitetee mbele ya waajiri na mashabiki wao. Bahati mbaya kwao referee alikuwa 'mwanamichezo'. Wakamiminiwa mabao kama nini sijui!
Sasa 'huyu mtu' anakuja na gia ya Wedi Kaap, ...who cares if he plays or not? Amuulize Joji Weah kama aliwahi kutia mguu Wedi kaap, ... aaaalah!!
Kwani asipokuwepo dunia itasimama? Tena akamuulize pia yule m'babe wa Sweden Ibrahimovic ambaye aliamini bila yeye mambo hayawezi kwenda, ... Mohamed Sallah inabidi abane mkia na kusukuma boll badala ya kuanza kujitafutia umaarufu kwa kufosi!