May 28, 2018


Klabu ya Azam FC imedhamiria kulipiza kisasi katika mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Yanga ili kumaliza ligi ikiwa nafasi ya pili.

Katika mchezo wa mzunguko wa kwanza uliopigwa kwenye Uwanja wa Azam Complex, Azam waliweza kutandikwa mabao 2-0 na Yanga.

Kichapo hicho wanakikumbuka Azam hivyo wamesema watapambana kufa kupona kuhitaji ushindi wa alama tatu kutoka kwa Yanga kwa lengo la kuweka heshima na kumaliza ligi wakiwa washindi namba mbili.

Kuelekea mechi hiyo itakayoanza majira ya saa 2 usiku, Ofisa wa Habari wa Azam, Jaffer Idd Maganga, amesema kuwa kikosi chao kimejipanga kwa ajili ya kupigania alama tatu muhimu kwa Yanga.

Maganga amefunguka kwa kueleza kwamba mechi hiyo haitakuwa rahisi kutokana na upinzani wa timu hizo pindi zinapokutana lakini wamejipanga kwa dhati ili kuhakikisha wanapata ushindi leo Jumatatu.

"Tunajua mechi ina upinzania mkubwa, tumejipanga kuhakikisha tunachukua nafasi ya umakamu bingwa na wachezaji wetu wamejiandaa kisawasawa" amesea Maganga.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic