BAADA YA KUMALIZANA NA PRISON, YANGA KUELEKEA MOROGORO LEO KUANZA KUKAMILISHA RATIBA
Kikosi cha Yanga kinaondoka leo jijini Mbeya kuelekea Morogoro kwa ajili ya mchezo wa ligi dhidi ya Mtibwa Sugar FC.
Yanga inaondoka jijini humo baada ya kukubali kufungwa jumla ya mabao 2-0 dhidi ya Tanzania Prisons jioni ya jana na kuzima rasmi ndoto za kuutetea ubingwa wa ligi.
Kikosi hicho ambacho kina wachezaji wengi wa timu B, kitakuwa na kibarua kingine kigumu dhidi ya Mtibwa Sugar katika Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro Mei 13 2018.
Mtibwa wametamba kufanya vizuri kuelekea mechi hiyo ambapo sasa wanaendelea na mazoezi wakiisubiri Yanga.
Kupoteza kwa Yanga jana kumeifanya Simba iwe bingwa rasmi wa Ligi Kuu yenye alama 65 ambazo haziwezi kufikiwa na timu yoyote ile na ikiwa imebakiza michezo mitatu kukamilisha ratiba.
Maskini Yanga!!!
ReplyDeleteLakini msikate tamaa. Mjitahidi kuchangishana ili hesabu itimie, kwani zile rufaa zaweza kuamshwa. Siku ile Lipuli ilicheza na Mbao, kipa wa Lipuli alivaa sox nyekundu - so jopo la wataalam likibana mkia na kuwawezesha Tiefuefu ni lazima watabatilisha matokeo ya ile mechi, na MWISHOWE mnyama atanyang'anywa pointi kumi na mbili (ndiyo - hakuna kishindikanacho kwa Yanga ikishirikiana na tiefuefu) yaani mechi zote ilizocheza na Lipuli na Mbao!
Hapo ubingwa huoooooo kwa maYebo, ... kiulainiiiii