May 11, 2018



Kikosi cha KRC Genk jana anachocheza Mtanzania, Mbwana Samatta, jana kilikwenda sare ya bao 1-1 dhidi ya KAA Gent katika mchezo wa Play Offs kwenye ligi ya Ubelgiji.

Samatta aliingia Uwanjani dakika ya 54 ya mchezo akitokea benchi kuchukua nafasi ya Mgiriki Nikolaos Karelia wakati timu yake ikiwa nyuma kwa bao 1-0.

Baada ya Samatta kuingia Uwanjani, ilimchukua takribani dakika 12 kuisawazishia Genk katika dakika ya 66 ya mchezo na mechi hiyo mpaka inamalizika matokeo yalikuwa ni 1-1.

Matokeo hayo yameifanya Genk kufikia jumla ya pointi 32 ikiwa imecheza jumla ya mechi 8 ikikamata nafasi ya 6.

2 COMMENTS:

  1. AISEEEE WE MUANDISHI KIBOKO, kwahiyo ligi ya UBELIGIJI, ukishinda mechi 1 unakuwa na pointi 4, maana nikichukua 32/8 napata 4....AISEE HONGERA SANA, NA KWA JINSI ULIVYO MMBEA UNGEKUWA UNAANDIKA HABARI ZA YANGA KUSAFIRI KWENDA ALGERIA KAMA YATIMA UNGEIANDIKA VIZURI, SHUBAAMITI

    ReplyDelete
    Replies
    1. tena hapo kuna sare pia hhhh

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic