May 28, 2018





Straika wa Ndanda FC, Mrisho Ngassa, amesema kuwa anashindwa kulala kutokana na kufikiria namna atakavyofanya kuisaidia timu yake kuepuka kushuka daraja.

Ndanda ipo kwenye hatari endapo itapoteza mchezo wa leo Jumatatu dhidi ya Stand United huku Majimaji ikipata ushindi dhidi ya Simba.

Ngassa alisema kuwa ana kazi kubwa kwa kushirikiana na wachezaji wenzake kuhakikisha kwamba wanaibuka na ushindi kwenye mchezo wao wa leo.

“Kazi kubwa tuliyonayo kwa sasa ni kuhakikisha tunapambana ili kuweza kushinda mchezo wa leo na kuweza kuinusuru timu yetu kushuka daraja kwa kuhakikisha kwamba tunafanikiwa kupata alama tatu muhimu na hicho ndicho kinachoninyima usingizi,” alisema Ngassa.

Kwa upande wa Kocha wa Stand United, Amars Niyongabo, alisema kuwa hana cha msalie mtume kwa timu ya Ndanda, atahakikisha anashinda mchezo huo kwa kuwa wachezaji wana morali ya kushinda.

“Kikubwa ni kuhakikisha mwamuzi anachezesha mpira kwa kuzingatia kanuni 17 za mpira hali itakayosaidia kumaliza kwa haki, tumejiandaa kwa ushindi, hilo ndilo tunalolitarajia kwa kuwa maelekezo yote nimewapa na mbinu za ushindi wanazo,” alisema Niyongabo.

SOURCE: CHAMPIONI

1 COMMENTS:

  1. Ngassa wa Yanga leo yupo kwenye timu inayonusulika kushuka daraja? Ama kweli usimtukane Mamba kabla hujavuka mto.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic