Baada ya siku chache kudaiwa kuwa, kiungo wa Simba, Mohamed Ibrahim ‘Mo’ amesajiliwa Yanga imebainika kuwa dili hilo linatarajiwa kukamilishwa rasmi leo Jumatano, baada ya pande mbili kukutana na kuweza kumalizana.
Mo tayari ni mchezaji huru kwa sasa kutokana na mkataba wake kumalizika mwezi ujao na amekuwa hana nafasi ndani ya kikosi cha Simba.
Meneja wa mchezaji huyo, Jamal Kisongo alisema anatarajia kukutana na viongozi wa klabu hizo ili kuweza kujadiliana.
“Suala la Mo litafahamika rasmi kesho (leo) sababu mchezaji alikuwa kwenye mechi kule Songea na leo Jumanne (jana) ndiyo anarejea hapa Dar kwa mapumziko, hivyo kila kitu kuhusu yeye kitajulikana tu baada ya kukutana pande mbili sababu alipata ofa kadhaa.
“Sababu mkataba wake na Simba ndiyo huo unamalizika na ligi imekwisha, hivyo tutajua mustakabali wake kwa ujumla msimu ujao utakuwa ni kwa klabu ipi na tunachohitaji ni mchezaji kupata timu na kuweza kuendeleza kipaji chake,” alisema.
CHANZO: CHAMPIONI
Kwaheri baba lakini usijekuwa miongoni wa wale watakaogoma kutokana na kukosa mshahara wako na ujiepushe na majuto endapo yatakukuta kwasababu majuto yanauwa. Itabidi uvumilie usiingie mitini madhali bado mpya katika kikosi chako kipya kama waliovumilia katika hicho kikosi cha yanga
ReplyDeleteHalafu utasikia wachezaji wetu wanasema wanandoto ya kucheza ulaya wakati kupigania number pale SIMBA kunamshinda yaani hovyo kabisa. Kama kigezo Kwenda Yanga ili kuitia pressure SIMBA pasi ningeomba viongozi wa SIMBA wamwuachie tu aende huko Yanga hata ajibu kaenda huko tulitarajia atabadilika lakini sioni kipya. Wakati mwengine hao mawakala wawe washauri wazuri wa hawa vijana kwanini unampeleka mchezaji kutoka SIMBA kwenda SIMBA hivi sasa si bora hata kupigania suala la kumpeleka kwa mkopo kwa timu kama mtibwa aende akajiulize alikosea wapi ili kujipanga upya.
ReplyDeleteTatizo vijana wakisifiwa na majukwaa basi wanataka makubwa zaidi ya kile wanacho deliver kwenye timu.Onyo alilompa kocha Lechntere ilibidi yeye na wakala wake walitafakari na kulifanyia kazi.Kwa mchezaji wa kujitambua na umri wake angeomba kutolewa kwa mkopo kwenye timu kama Mtibwa ambako kuna utulivu ili ajifunze kile allichokosea.Lakini huwezi kumlaumu lazima tuangalie na upande wa pili wa shillingi maana pengine alishachukua pesa mapema toka Yanga.Ikabaki mchezaji kutojituma na kuchezea klabu ili mradi tu akisubiria mkataba uishe.Kwa viongozi wa Simba msihangaike naye mwacheni aende anako ona atapasua ili mradi asiache kuangalia maendeleo ya wenzake waliondoka kwa mashinikizo kina Ajib, Singano.Ule msemo wa mtoto akililia umpe ukimkata ndio atajua machungu yake
ReplyDeleteTatizo vijana wakisifiwa na majukwaa basi wanataka makubwa zaidi ya kile wanacho deliver kwenye timu.Onyo alilompa kocha Lechntere ilibidi yeye na wakala wake walitafakari na kulifanyia kazi.Kwa mchezaji wa kujitambua na umri wake angeomba kutolewa kwa mkopo kwenye timu kama Mtibwa ambako kuna utulivu ili ajifunze kile allichokosea.Lakini huwezi kumlaumu lazima tuangalie na upande wa pili wa shillingi maana pengine alishachukua pesa mapema toka Yanga.Ikabaki mchezaji kutojituma na kuchezea klabu ili mradi tu akisubiria mkataba uishe.Kwa viongozi wa Simba msihangaike naye mwacheni aende anako ona atapasua ili mradi asiache kuangalia maendeleo ya wenzake waliondoka kwa mashinikizo kina Ajib, Singano.Ule msemo wa mtoto akililia wembe....mpe ukimkata ndio atajua machungu yake
DeleteMaskini Singano anatia huruma sana. Hatabiriki lini anachezeshwa hana uhakika tofauti na alipokuwa Simba, alikuwa winga wa uhakika. Wakati mwingine vijana vumulieni kukaa na kukulia sehemu inayokupa nafasi ya kucheza. Simba imewalea vizuri vijana hawa.
DeleteSasa Mo wakiungana na Hajib na Ishaka mambo yamekwisha na ubingwa na kombe la Africa kwenda yanga tu
ReplyDeleteMasikini yeye mwenyewe kwa hiari yaki anajopeleka shimoni amba wengine ambapo wengine wanatapatap kuitafuta njia ya kutoka. Si ajabu ikiwa Mo anaingia na Uondani ana haki ya kujikwamuwa
ReplyDeleteSasa Yanga bwana hawataki masiara piga nikupige Hela itakuwepo na katika mkutano ujao wameambiwa kila mjumbe atelemshe mkwanja wa shilingi 30,000 basi unaona mshikimano kwa Mo usifanye ofu utapata tu mshaala wako na huko na aliyekupeleka uko ndie ataekupatia nafasi za nje kama kama walivopata wengine na kurejea tajiri
ReplyDeleteMo Ibrahim nimchezaji mzuri sana tatizo ni yeye mwenyewe aliporuhusu starehe kuingiliana na mazoezi ya mpira na kuanza kuwa na ratiba yake mwenyewe ya kwenda mazoezini. Kama tunakubali vijana bado walelewe na kuvumiliwa basi Meneja wake anapaswa amsaidie Mo kwenye kujitambua. Kwakweli mimi binafsi nilimpenda sana Mo uchezaji wake ana kipaji cha hali ya juu. Mo akitullia na kujitambua atarudi yule yule. Anao uwezo mkubwa tu. Mungu akubaliki sana Mo daima Simba itakuwa tayari kukupokea.
ReplyDelete