CHUJI ATOFAUTIANA NA WENGINE, AWATAJA WAAMUZI WASAIDIZI KUWA BORA SIMBA VS YANGA
Na George Mganga
Mchezaji wa zamani wa Simba na Yanga, Athuman Idd 'Chuji, amefunguka kuhusiana na namna alivyoutazama mchezo uliowakutanisha watani wa jadi juzi Jumapili akieleza kuwa haukuwa na burudani.
Chuji ameeleza kuwa mechi hiyo ilikuwa ni ya piga ni kupige zaidi kuliko kuonesha soka likitandazwa Uwanjani, hali iliyopelekea kushindwa kuonesha mpira wa ambao ungeweza kukonga mioyo ya mashabiki waliohudhuria Uwanjani.
Akizungumza kupitia kipindi cha Sports Xtra, Clouds FM, Chuji alieleza kuwa Simba walipata nafasi moja pekee na kuweza kuitumia, nafasi ambayo ilikuwa ni adhabu ya faulo iliyopigwa na Shiza Kichuya kisha kuzaa bao hilo lililofungwa na Erasto Nyoni kwa kichwa.
Mchezaji huyo aliyewahi kuzicheza timu hizo mbili, alisema hakuona mpira wa burudani kitu ambacho kwake anaamini ulipoteza utulivu.
Aidha, Chuji amesema hakuona mchezaji bora katika mchezo huo huku akiwataja Waamuzi Wasaidizi kuwa ndiyo bora katika dakika zote 90 za mtanange huo.
Ahsante teknolojia!Kabla ya uwepo wa teknolojia tulilishwa sana matango pori.Mpira unachezwa hadharani na sote tumeona namna soka lilivyopigwa,anapotokea mtu mmoja na kusema walicheza butuabutua huku watazamaji tuliona namna Simba ilivyokuwa inachora michoro uwanja mzima ni kutukosea adabu watazamaji.
ReplyDeleteTuweke ushabiki pembeni,Simba ilitengeneza nafasi nyingi sana za magoli,japo walishindwa kuzitumia,kusema eti walitengeneza nafasi moja tu ni kuyadhurumu macho yako yaliyoshuhudia soka lile.
Unaweza kucheza mpira kiwango cha juu lakini moshi wa bangi ukadanganya macho yako. Jamaa alitaka kiki tu, na ameumia timu lake kufungwa. Timu inacheza kwa maelekezo ya mwalimu, game plan ya simba ilifanikiwa na kusema hakuna mchezaji aliyecheza vizuri ni upuuzi wa kupuuzwa. Kwakifupi jamaa ameumizwa na matokeo ila sayansi ya soccer haijui zaidi ya kucheza kwa mazoea. Pole kwake kwa kuonyesha kuwa ana chuki na wengine.
ReplyDeleteUsimchukulie seriously mtu ambae aliapa kuwa bora auze ndimu kuliko kucheza Simba, halafu akasahau na kurudi tena Simba. Tutakutana naye uwanjani next season tuone yeye akiwa man of the match.
ReplyDeleteChuji ameonesha upeo mdogo sana katika kuchambua mpira mi nadhani sio yeye ni mahaba yake tu kwa yanga
ReplyDeleteBangi mbaya sana ndo maana wengine wanatokaga mchana na kibatari wanajua kuna giza
ReplyDeleteni maoni yako lkn ukumbuke mechi hiyo iina mengi sana hasa kwa kuwa ni mechi kubwa ikiwemo tensions nk hata chuji aliwahi kutuhumiwa kucheza kiwango cha chini mechi ya watani
ReplyDeleteChino akistaafu soka kamwe asijihusishe na kazi YA uchambuzi wa soka, ataaibika kwani hana upeo huo.Dunia kwani sasa iko kiganjani, wote tuliuuona mpira live SIMBA walitandaza soka LA uhakika na yanga nao walijaribu kuiga na kuacha mpira wao wa kubutua butua
ReplyDelete