May 27, 2018


Mshambuliaji wa kimataifa wa Liverpool, Mmisri, Mohammed Salah, amesema hatoweza kujiunga na Real Madrid kutokana na mchezo ambao si wa kiungwana waliouonesha jana wakati wakicheza mechi ya fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya huko Ukraine.

Salah ameeleza kusikitishwa zaidi na tukio la nahodha wa Real Madrid, Sergio Ramos kwa kitendo chake cha kumuumiza mkono na kupelekea kuondolewa nje ya Uwanja baada ya kushindwa kuhimili maumivu.

Mchezaji huyo amesema kitendo kama hicho ni mbinu chafu za kujitafutia matokeo badala ya kucheza mpira ambao unafuata sheria zote 17 za mchezo wa soka.

Kuafuatia rafu iliyopelekea kuumia mkono wake, Salah amesema hataweza kujiunga na timu hiyo ambayo imeonesha nia ya dhati kutaka kumsajili hivyo ataendelea kusalia Liverpool na si kwenda Madrid.

Katika mchezo huo uliopigwa mjini Kiev, ulimalizika kwa Real Madrid kuibuka na ushindi wa mabao 3-1 na kuweza kubeba taji la tatu mfululizo katika UEFA Champions League.

3 COMMENTS:

  1. Ustadh naona ka hamaki kwani hata Real Madrid nao fullback wake ameumizwa pia he he so wajipange kisha bado hajafika level hiyo ya kujinadi kutokwenda Real Madrid coz hata Messi behind the camera atakwambia ana ndoto ya kucheza real

    ReplyDelete
    Replies
    1. ongea soka si ushabiki Carvajol aliumizwa na nani aliumia mwenyewe hakuvutwa maksudi kama salah

      Delete
    2. Sallah kajiangusha tu mwenyewe pia. Hakusukumwa. Alikuwa na hofu ya kutoweza kufunga na kuisaidia timu yake ishinde, hivyo akaamua kutafuta mbinu ya kutoka uwanjani mapema.

      Dhoruba kama hoyo hata mtu ambaye hakufanya mazoezi kwa miezi sita haiwezi kumuumiza.

      Imekuwa kwake, na kwao pia.

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic