May 24, 2018
Jumamosi Mei 19,2018 tulikuwa na tukio kubwa la sherehe za kukabidhi Kombe la Mshindi wa pili Kombe la Dunia la Watoto wa Mtaani, Ubingwa wa Cecafa kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kukabidhi Kombe la Ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.

Kwa namna ya kipekee kwa niaba ya TFF napenda kumshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.Dkt John Pombe Magufuli kwa kukubali ombi letu la kuwa mgeni rasmi katika tukio hilo. 

Tumefarijika kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania MH.John Pombe Magufuli kuungana na Wanamichezo na kuzungumza nao.

Alichozungumza Mh.Rais Magufuli tumekipokea na tunaahidi tutakifanyia kazi kwa vitendo katika kuunga mkono jitihada zake za dhati kuona mpira wa miguu unapiga hatua. 

Tunaamini Wanamichezo wengine nao wataunga mkono jitihada hizo za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na jitihada za TFF ili kufanikisha lengo. 

TFF tutahakikisha tunasimamia mpira wa Tanzania kwa kuongozwa na sheria,kanuni na utaratibu na hatutakubali kuona mtu anakwenda kinyume na kutaka kuvuruga taswira nzuri ya Mpira tuliyoanza kuijenga katika kipindi kifupi tulichoingia madarakani. 

Tunaamini ushirikiano wetu na Serikali ya awamu ya Tano chini ya Mh.Rais John Pombe Magufuli tutafikia lengo kwa pamoja. 

Serikali ya awamu ya tano imekuwa na ushirikiano mkubwa na TFF katika kufanikisha masuala mbalimbali ushirikiano ambao hakika utaleta matunda zaidi. 

Tunaamini kuwa timu zetu za Taifa zitafanya vizuri kama ambavyo timu yetu ya Vijana U17 Serengeti Boys ilivyofanya vizuri na kuchukua Kombe nchini Burundi na timu ya Wasichana ya kituo cha TSC nao walivyofanya vizuri na kufika fainali kombe la dunia la Watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu. 

Hakika ni mfano wa kuigwa mpaka kwenye ngazi ya klabu kwa kushinda mataji mbalimbali.

Mwisho namuhakikishia Mh.Rais Magufuli tutaendelea kusimamia mpira wetu ipasavyo kwa kushirikiana na Serikali  kwenye kila eneo linalohitaji msaada wa serikali.


Cliford Mario Ndimbo 
Afisa Habari na Mawasiliano TFF 
Mei 24,2018

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV