SIMBA YAMNASA STAA HUYU KUTOKA MAJIMAJI FC
Na George Mganga
Kabla ya hata ya Ligi Kuu Bara kumalizika taarifa zinaeleza kuwa mabosi wa Simba tayari wameshamalizana na nyota wa Majimaji FC, Marcel Kaheza kwa kusaini naye mkataba wa awali wa miaka miwili.
Kaheza ambaye aliwahi kuichezea Simba B na kikosi cha kwanza kisha kuchukuliwa kwa mkopo na Majimaji na baadaye baadaye kumsajili, ameonesha kiwango kikubwa msimu huu kwa kufunga idadi ya mabao 13 akiachwa na Okwi aliyefikisha 20.
Mbali na idadi hiyo ya mabao, Mshambuliaji huyo amefanikiwa kutwaa tuzo ya mchezaji bora wa Ligi Kuu Bara kwa mwezi Aprili 2018.
Kaheza alitwaa tuzo hiyo baada ya kuwashinda wenzake wawili, John Bocco na Emmanuel Okwi wote wa Simba ya Dar es Salaam katika uchambuzi uliofanywa wiki hii na kamati ya tuzo hizo.
Wakati Majimaji FC ikiwa inajiandaa kucheza na Simba Jumatatu ya wiki ijayo, inaelezwa mchezaji huyo hatokuwa sehemu ya kikosi kutokana na kusajiliwa na Simba.
simba mnanipa raha sana.hy ni mashine.anakipaji sana huyu dogo.
ReplyDeletesimba mnanipa raha sana.hy ni mashine.anakipaji sana huyu dogo.
ReplyDeleteMwendo uwe wa kasi hiyo na ikiwezekana Salamba pia chonde madhali mmeshajitokeza kati ya chaguo mnaowataka pia atatupa raha na furaha asiachwe katika kinyanganyiro. Kila la heri huu ndio mwaka wa mnyama
ReplyDelete