BAADA YA YONDANI KUMTEMEA MATE ASANTE KWASI, TFF YATOA TAMKO
Kuafuatia kitendo cha mchezaji na beki wa Yanga, Kelvin Yondani, kumtemea mate Asante Kwasi katika mchezo wa ligi dhidi ya Simba, Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limetoa tamko.
Kupitia Afisa Habari wa TFF, Clifford Mario Ndimbo, amesema kuwa bado hawajapokea malalamiko kutoka Simba kuhusiana na suala hilo.
Mbali na ripoti kutoka Simba, Ndimbo ameeleza kuwa wao hutegemea pia ripoti ya Kamisaa wa mchezo husika ili kuja kuifanyia tathmini na kuja wapi kulikuwa na mapungufu ili yaweze kufanyiwa kazi.
Akizunguza jana jioni, Ndimbo amesema kuwa kama Simba watafikisha malalamiko yao, taratibu zingine za kihatua zitafuata ila kwa sasa hawawezi kufanya chochote.
Katika mchezo huo uliopigwa juzi Jumapili, Yondani alionekana kumtemea mate Kwasi ambaye hakuonesha kujibu mapigo ikiwa ni kipindi cha kwanza cha mchezo.
kushugurikia kitu hadi mpewe malalmiko wakati kile kitendo kila mtu alikishuhudia mbona Juma Nyoso hamkusubiri na hiyo kamati yenu ya masaa 72 inafanyaje kazi
ReplyDeleteNi jambo la kushangaza kwa Tff ya tangu uwepo wa Malinzi mpaka leo wakati wa karia eti kamati ya Saa 72 baada ya mchezo inapita mwezi zaidi ya mmoja ndio inatoa maamuzi. Nyosso alimdhalilisha Bocco suala lake likapewa uzito sana hata kabla ya hiyo kamati ya SAA 72 tayari Tff ilishaingilia kati leo kitendo cha Yondani kumtemea mate Kwasi wanajifanya hawajaona sasa kuna umuhimu gani wa kusema yupo mdhamini wanayemtambua anayerusha matangazo mubashara kwamba hata TV hawafuatilii au ndio mahaba?
ReplyDeleteHuu ni uzwazwa wa hali ya juu sana. Kwa hiyo kosa ni kosa pale mtendewa kosa napolalamika? Je, kama Simba wakiamua kumsamehe Yondani, basi kutakuwa hakuna kosa? Mbona matendo ya kishirikina mnayatolea maamuzi? Je, timu huwa zinalalamikia mambo hayo? Match Observer akisema kitendo hicho kilitokea na ripoti ya mwamuzi isiseme chochote kuhusu kitendo hicho, ina maana hakuna kosa? Jifunzeni kwa wenzetu, wao huwa hawasubiri mashitaka, bali kuna matendo ambayo huwa waamuzi hawayaoni wala match observer lakini hutolewa maamuzi na adhabu huchukua mkondo kwa aliyefanya hivyo. Kwani msiunde kamati maalumu ya ku-review mchezo mzima kwa kutumia picha za televisheni na kutolea maamuzi masuala kama hayao?
ReplyDeleteSimba iiwasilisha malalamiko ya Ngoma kumpiga Hassan Kessy TFF walifanya nini?
ReplyDeleteBanda alimpiga ngumi George Kavilla, Refa hakuona lakini TFF ilimfungia miaka miwili bila Kagera kuwasilisha malalamiko...DOUBLE STANDARDS
Hata tukio la Yondani kwa Bocco maamuzi yalitokana na PICHA TU
Delete"Spitting is disgusting at all times. It's unhygienic and unhealthy, particularly if you spit close to other people," said an HPA spokesman. "Footballers, like the rest of us, wouldn't spit indoors so they shouldn't do it on the football pitch.
ReplyDelete"If they are spitting near other people it could certainly increase the risk of passing on infections. Spitting is a nasty habit that should be discouraged – and it should be discouraged by the clubs. It's about setting examples for young people who idolise footballers."
The spokesman added that footballers should follow the same guidelines as other members of the public by washing their hands, covering their mouth when sneezing and disposing of used tissues. "The advice is catch it, bin it, kill it," he said.
The Football Association and Premier League said they were following guidance from health experts in handling the issue. "As ever, when it comes to health matters the Premier League will be guided by the relevant statutory authorities," said a Premier League spokesman.
Ikiwa ni hivo, basi hata polisi wakimkuta mwizi anaiba, mwizi huyo asichukuliwe hatua mpaka aliyeibiwa apeleke malalamiko ya kuibiwa
ReplyDelete