YANGA KUMKOSA MCHEZAJI MMOJA DHIDI YA RAYON KESHO
Na George Mganga
Kikosi cha Yanga kesho kitakuwa na kibarua kizito kitakapokabiliana na Rayon Sports ya Rwanda katika mchezo wa Kmbe la Shirikisho Afika.
Wapinzani wa Yanga tayari wamewasili jana nchini kwa ajili ya mchezo huo wa pili katika hatua ya makundi ya mashindano haya.
Kuelekea mechi hiyo, Yanga itakosa huduma ya mchezaji wake, Said Makapu kutokana na kutumikia adhabu ya kadi 2 za njano ambazo kwa mujibu wa kanunu za mashindano, mchezaji anapaswa kukosa mechi moja endapo atafikisha idadi ya kadi hizo.
Yanga itamkosa Makapu katika mtanange huo huku ikitakiwa kupambana kupata matokeo ambayo yataitengeneza mazingira mazuri ya kuendelea kusalia kwenye michuan hiyo ya Kombe la Shirikisho Afrika.
Kuelekea mechi hiyo, salehjembe.blogspot.com inawatakia kila la kheri Yanga dhidi ya Rayon Sports ya Rwanda.








Naungana na Saleh Jembe kuwatakia YANGA kila la heri
ReplyDeleteAll the best yanga
ReplyDeleteTufuteni machozi watanzania Yanga
ReplyDeleteProtas-Iringa
If Prison 2 Yanga 0 and Mtibwa 1 Yanga 0 that means 2+1 = 3 Therefore, Rayon 3 Yanga 0.
ReplyDeleteI will all the Best Rayon Sports