June 21, 2018


Na George Mganga

Beki aliyekuwa akiichezea Kagera Sugar, Mohamed Fhaki, amejiunga na klabu mpya iliyopanda daraja kushiriki Ligi Kuu msimu ujao, JKT Tanzania.

Taarifa zinaeleza tayari mchezaji huyo ameshamalizana na mabosi wa JKT Tanzania ambao wamedhamiria kufanya vizuri kuelekea msimu mpya unaotarajiwa kuanza mwezi Agosti.

Fhaki alijizolea umaarufu mkubwa msimuwa 2016/17 kutokana na sakata la kudaiwa kuwa alikuwa na kadi za njano baada ya Simba kutuma malalamiko yao TFF wakiomba wapatiwe alama tatu na mabao matatu baada ya mechi dhidi ya Kagera ambayo Simba walifungwa 2-1 ugenini.

Mchezaji huyo ametua JKT na kusaini mkataba wa miaka miwili ambao utakuwa unamalizika mwaka 2020.

Usajili huo wa JKT umekuwa ni moja ya maandalizi kuelekea msimu ujao wa ligi ambao utahusisha jumla ya timu 20 tofauti na 16 ambazo zilikuwepo mwanzo.

1 COMMENTS:

  1. Halafu sijaelewa sababu ya wewe kuandika eti Fakhi aliwanyima simba alama za mezani.inajulikana walioinyima simba alama wako mahabusu..Unakuwa biased mwandishi

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic