June 21, 2018



Dakika 90 zimemalizika huko Urusi katika michuano ya Kombe la Dunia kwa Denmark kwenda sare ya bao 1-1 na Australia.


Mabao ya mchezo huo yamefungwa na Christian Eriksen mapema kabisa mnamo dakika ya 7 kipindi cha kwanza kwa upande wa Denmark. 

Bao la Australia limewekwa kimiani na Mile Jedinak kwenye dakika ya 38 kwa njia ya penati ikiwa ni baada ya Yussuf Poulsen kuunawa mpira katika eneo la hatari na kusababisha kupewa kadi ya njano.

Matokeo haya yanaifanya Denmark kuendelea kushika nafasi ya kwanza kwenye kundi C ikijikusanyia alama 4 huku Australia ikiwa na alama 1 katika nafasi ya 4.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic