June 23, 2018


Beki wa kulia wa klabu ya Yanga, Hassan Kessy, amefunguka kuhusiana na mustakabali wa mkataba wake na klabu.

Mchezaji huyo tayari ameshamaliza mkataba wake na sasa yupo huru kuelekea popote pale kucheza soka.

Imeelezwa kuwa Kessy ambaye aliwahi pia kuichezea Simba amefunguka na kusema kwa sasa yeye anazidi kujiweka fiti zaidi ili kiwango chake kisishuke.

Aidha, Kessy ameeleza suala la mkataba anahusika nalo Meneja wake ambaye anamsimamia zaidi, hivyo ikitokea amepata dili la kucheza, isije ikawa tabu kuonesha kile alichonacho miguuni.

Haijajulikana kama Kessy ataendelea kusalia Yanga ingawa mabosi wa klabu hiyo hivi karibuni walinena wapo kwenye mazungumzo na wachezaji ambao mikataba yao imeshamalizika.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic