June 23, 2018


Kikosi cha klabu ya Simba kinaingia tena mwindoni leo kujiandaa na mashindano ya Kagame yanayoanza Juni 28 wiki ijayo jijini Dar es Salaam.

Wachezaji baadhi wa Simba jana walianza rasmi mazoezi baada ya mapumziko ya wiki kadhaa ambayo walikuwa wamepewa na uongozi wao.

Simba wataendelea na mazoezi hayo leo kwenye Uwanja wa White Sand uliopo maeneo ya Mbezi Beach Dar es Salaam.

Wakati huo Simba wakiendelea kujifua, inaelezwa mabosi wa klabu hiyo wako kwenye mpango wa kumsaka beki mmoja wa kimataifa.

Jina la Pascal Wawa aliyewahi kuichezea Azam FC miaka kadhaa iliyopita limehusishwa kuwa kwenye rada za mabosi wa Simba ili aweze kurejea kuongeza makali ya ulinzi.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic