JINGINE LA USHIRIKI WA MTIBWA KATIKA MASHINDANO YA CAF, TFF WAFIKIA HATUA HII KULIKAMILISHA
Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kupitia kwa Kaimu Katibu Mkuu, Wilfred Kidao, limesema kuwa linasubiria majibu ya CAF kuhusiana na ushiriki wa Mtibwa Sugar katika mashindano ya Kombe la Shirikisho Afrika.
Mtibwa wanasubiria hatima yao ya ushiriki baada ya kifungo cha miaka mitatu kufutia kushindwa kujikimu kusafiri kuelekea nje ya nchi ili kushiriki mashindano ya Ligi ya Mabingwa Afrika wakati ikiwa bingwa wa ligi, mwaka 2000.
Kidao amesema kuwa tayari walishatuma barua ya kuelekea CAF wakitaka kujua kama Mtibwa inaweza ikashiriki mashindano hayo baada ya adhabu ya miaka mitatu waliyokuwa wamefungiwa kumalizika.
Mtibwa wanajiuliza kuhusiana na kushiriki mashindano hayo baada ya kupata nafasi kutokana na ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Singida United kwenye mchezo wa Kombe la TFF uliopigwa Uwanja wa Sheikh Amri Abeid.
"Ni kweli tumeshatuma barua CAF kusubiri majibu juu ya Mtibwa, sasa tunasubiria majibu tu na hilo ndiyo lilobaki" alisema Kidao.
0 COMMENTS:
Post a Comment