JOACHIM AINGIA LAWAMANI BAADA YA KUACHA KUMJUMUISHA SANE KIKOSI CHA TIMU YA TAIFA
Gumzo kubwa limeibuka mitandaoni kwa wadau wa soka kuhoji juu ya Kocha wa timu ta taifa ya Ujerumani, Joachim Low kuacha kumwita kikosini winga wa Manchester City, Leroy Sane.
Sane, Mlinda mlango wa Bayer Leverkusen, Bernd Leno na Jonathan Tah pia mshambuliaji wa Freiburg Nils Petersen ni miongoni mwa wachezaji walioachwa.
Hoja kubwa imeibuka kufuatia kuachwa kwa wachezaji hao haswa Sane ambaye amenga'ra vizuri ndani ya Manchester City katika msimu wa Ligi Kuu England uliomalizika (2017/18).
Mshangao umekuja kwa wengi ikiwa ni baada ya Sane kuachwa huku golikipa Manuel Nuer aliyekosekana Uwanjani kwa takribani miezi 9 akiwa majeruhi kujumuishwa kwenye orodha ya wachezaji 23 watakaokipiga kwenye michuano ya Kombe la Dunia huko Urusi.
Lawama nyingi zimetupiwa kwake na pengine yawezekana kama timu isipofanya vizuri anaweza akalaumiwa zaidi.
Wachezaji kwa ujumla walioitwa na Kocha Joachim Low ni hawa hapa:-
Makipa: Manuel Neuer (Bayern Munich), Marc-Andre ter Stegen (Barcelona), Kevin Trapp (Paris St-Germain)
Mabeki: Jerome Boateng (Bayern Munich), Matthias Ginter (Borussia Monchengladbach), Jonas Hector (Cologne), Mats Hummels (Bayern Munich), Joshua Kimmich (Bayern Munich), Marvin Plattenhardt (Hertha Berlin), Antonio Rudiger (Chelsea), Niklas Sule (Bayern Munich)
Viungo: Julian Brandt (Bayer Leverkusen), Julian Draxler (Paris St-Germain), Leon Goretska (Schalke), Ilkay Gundogan (Manchester City), Sami Khedira (Juventus), Toni Kroos (Real Madrid), Mesut Ozil (Arsenal), Sebastian Rudy (Bayern Munich)
Washambuliaji: Mario Gomez (Stuttgart), Thomas Muller (Bayern Munich), Marco Reus (Borussia Dortmund), Timo Werner (RB Leipzig)
0 COMMENTS:
Post a Comment