June 23, 2018


Taarifa ambazo ziko chini ya kapeti zinaeleza kuwa kipa Juma Kaseja amejiunga na KMC FC kwa kusaini mkataba wa mwaka mmoja.

Kaseja ambaye alikuwa akiichezea Kagera Sugar msimu uliomalizika, ameamua kuachana na walima miwa hao wa Kaitaba na kutimkia KMC iliyopanda kucheza Ligi Kuu msimu ujao.

Licha ya viongozi wa KMC kuonekana hawataki kuweka wazi juu ya suala hili, lakini taarifa za ndani zinaeleza tayari wameshalizana na Kaseja.

KMC imeanza maboresho ya kikosi chao ili kuhimili vishindo vya Ligi Kuu Bara ambayo itakuwa moto zaidi msimu huu kutokana na jumla ya timu kuwa 20.

Kipa huyo alijizolea umaarufu mkubwa Tanzania kutokana na umahiri wake langoni haswa wakati akiwa anaichezea Simba SC.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic