June 23, 2018


Kocha Msaidizi wa Simba, Masoud Djuma, ameamua kuileta Simba kivingine kuelekea michuano ya KAGAME inayotaraji kuanza wiki ijayo Juni 28.

Mrundi huyo ambaye amechukua mikoba kwa muda ya Mfaransa Pierre Lechantre, ameamua kikosi chake kufanya mazoezi mara mbili kwa siku ili kukiweka fiti zaidi kabla ya mashindano kuanza.

Djuma amefunguka na kueleza sababu kubwa ya kufanya hivyo ni kurejesha makali ya Simba kama iliyoanza nayo baada ya kuanza kukinoa kikosi ikiwa ni siku kadhaa baada ya Mcameroon, Joseph Omog kuondoshwa.

Kocha huyo amesema wiki hii itakwenda namna hiyo na ikiwezekana kuanzia wiki lijalo kikosi kinaweza kuanza mazoezi ya mara moja kwa siku.

Kikosi hicho kimefanya mazoezi leo asubuhi kwenye Uwanja wa White Sand jijini Dar es Salaam na baadaye jioni kitaendelea tena kujinoa.



0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic