Wakati ikielezwa kuwa Yanga wapo kwenye harakati za kutaka kumrejesha kiungo wao wa zamani Hassan Dilunga anayeichezea Mtibwa Sugar, Azam nao wameanza mipango ya kumuwania kipa wao, Benedicto Tinocco, imeelezwa.
Tinocco ambaye aliwahi kusajiliwa Yanga na kushindwa kupata nafasi ya kuichezea klabu hiyo kutokana na uwepo wa Deo Munish na Ally Mustapha kipindi hicho, ameingia kwenye rada za Azam kutokana na mchango mkubwa alionesha ndani ya Mtibwa msimu uliomalizika.
Tinocco amekuwa kipa tegemo wa Mtibwa hivi sasa aliyechukua nafasi ya Said Mohamed ambaye ni kipa wa akiba kwenye klabu ya Simba, amefanya vizuri pia katika ligi msimu uliomalizika.
Tetesi za usajili huu zinaonesha nia ya dhati kwa Azam ya kumpa tafu kipa wake wa sasa, Mghana, Razak Abalora ambaye amekuwa sehemu ya kikosi cha kwanza kwa muda mrefu.
Kazi ya ziada itakuwepo kwa Tinocco ambaye kama atatua Azam kupigania namba na Abalora pamoja na Mwadini Ally ambaye ni kipa namba mbili.









0 COMMENTS:
Post a Comment