June 24, 2018


England imeonesha ubabe wa kutosha katika mchezo wa kundi G dhidi ya Panama kwa kuipa kipio kikali cha mbwa koko cha mabao 6-1 kwenye michuano yaKombe la Dunia nchini Urusi.

Mabao matatu ya England yamewekwa kimiani na Harry Kane ambapo amefunga mawili kwa njia ya penati.

Mabao mengine ya England yamewekwa kimiani na John Stones aliyefunga mawili huku Jesse Lingard naye akitupia moja.

Panama imejipatia bao pekee la kufutia machozi kupitia kwa Nahodha wake, Felipe Baloy mnamo dakika ya 78.

Matokeo hayo yanaifanya Panama kuaga rasmi mashindano hayo na kuiacha England ikifikisha alama 6 mpaka nafasi ya kwanza ikiiacha Ubelgiji kwa utofauti wa mabao ya kufuna na kufungwa.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic