June 12, 2018


Real Madrid wamewasiliana na meneja wa zamani wa Chelsea na Tottenham Andre Villas-Boas kuchukua mahala pake Zinedine Zidane. (RMC Sport - in French)

Baada ya kuwapata Mauricio Pochettino na Harry Kane kwa mikataba wa muda mrefu, Tottenham wanakaribia kukubaliana mkataba mpya na mchezaji Dele Alli,22, wa thamani ya paunia 100,000 kwa wiki. (London Evening Standard)

Liverpool huenda wasitoe ofa ya kumsaini kipa wa Brazil Alisson, 25, kutoka Roma. (Sky Sports)

Alisson anataka hatma yake kutatuliwa kabla ya Brazil kuanza kampeni yake ya Kombe ya Dunia dhidi ya Swizerland siku ya Jumapili. (ESPN)

Kiungo wa kati wa Italia Jorginho, 26, yuko tayari kubaki Napoli lakini kuhamia Manchester City itakuwa fursa ya kihistoria kwa mchezaji huyo kulingana na ajenti wake . (TuttoMercatoWeb via Four Four Two)

'Sergio Ramos ana bahati hatutakutana uwanjani'
Arsenal wako kwenye mazungumzo ya kumsaini kiungo wa kati wa Sampdoria Lucas Torreira, 22, kwa pauni milioni 22 ambaye anaichezea Uruguay kwenye kombe la dunia. (Mail)

Fiorentina wameongeza ofa yao ya kumunnua mchezaji wa kimataifa wa Italia Federico Chiesa, 20, hadi pauni milioni 62m - wakati pia anamezewa mate na Liverpool, Manchester City na Manchester United. (Gazzetta dello Sport, via

Meneja wa Jose Mourinho anataka kumsaini mchezaji mmoja zaidi kabla ya Kombe la Dunia na huenda akaanza kumtafuta mlinzi wa Tottenham wa thamani ya pauni milini 50 Toby Alderweireld. (Sun)

Kutoka BBC

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV