July 11, 2018


Na George Mganga

Wakati vuguvugu la usajili wa wachezaji Tanzania kutoka klabu moja kuelekea nyingine likiendelea kushika kasi nchini Tanzania, uongozi wa Mtibwa Sugar umefunguka juu ya uvumi wa kiungo wake, Hassan Dilunga kuhusishwa kutua Simba.

Kupitia Katibu Mkuu wa klabu hiyo, Jamali Byser, ameeleza kuwa wao kama klabu hawana mpango wa kumuachia mchezaji huyo akisisitiza kuwa hakuna uwezekano huo maana wanamtegemea kwa sasa.

Kwa mujibu wa Radio One kupitia kipindi cha michezo, Byser ameweka wazi kuwa yanayoongelewa ni tetesi tu na hakuna ukweli wowote wa Dilunga kutimkia kwa mabingwa hao wapya wa Ligi Kuu Bara msimu wa 2017/18.

"Ni tetesi tu hizo, bado tunahitaji kuwa naye kutokana na mchango wake kama mchezaji, hatuwezi kuruhusu akaondoka" alisema.

Byser amesema Dilunga ana mkataba wa mwaka mmoja ambao bado haujamalizika na akisema wanaendelea kufana naye mazungumzo ili kama itawezekana aweze kuongeza mwingine.

Ikumbukwe Dilunga ameanza kuhusishwa takribani wiki kadhaa sasa kutua Simba huku Yanga pia nao wakitajwa kuwa wanahitaji kumrejesha klabuni kwao.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic