BAADA YA KUSAJILI KIPA MWINGINE, ROSTAND KUPELEKWA TIMU HII KWA MKOPO
Hatimaye kibarua cha kipa Mcameroon Youthe Rostand katika kikosi cha Yanga kimeota mbawa baada ya mabosi wake kuonesha nia ya kumpeleka kwa mkopo kwenye klabu ya zamani.
Taarifa kutoka ndani ya Yanga zinasema uongozi wa juu upo kwenye mazungumzo ya mwisho na African Lyon kwa ajili ya kuwapa Rostand kwa mkopo ili ajifue upya kuimarisha kiwango chake.
Hatua hiyo imefikiwa mara baada ya usajili wa kipa mwingine Mkongo, Nkizi Kindoki kutoka klabu ya Racing da Kinshasa.
Kindoki ametambulishwa jana mbele ya waandishi wa habari kunako makao makuu ya klabu hiyo ambapo sasa atakuwa pamoja na Ramadhan Kabwili.
Wakati Yanga wakiwasiliana na Lyon, inaelezwa kuwa Rostand hataki kupelekwa kwa mkopo na badala yake amewataka mabosi wake kumpa chake ili aweze kuelekea mahala pengine.








0 COMMENTS:
Post a Comment