July 8, 2018


Baada ya kumalizana na Juma Abdul pamoja na Deus Kaseke, uongozi wa klabu ya Yanga umefanikiwa kuingia mkataba mpya na kipa wake, Beno Kakolanya.

Kakolanya aliyekuwa kwenye mazungumzo na uongozi wa Yanga kupitia kwa Meneja wake, Seleman Haroub, wamefikia makubaliano ya kusaini mwaka mmoja na mabingwa hao wa kihistoria katika Ligi Kuu Bara.

Beno ambaye alisajiliwa kutoka Tanzania Prisons, ameamua kuweka kandarasi hiyo ya mwaka mmoja na sasa atakuwa sehemu ya kikosi cha Yanga kuelekea msimu ujao wa Ligi Kuu.

Mbali na Kakolanya, mabosi wa Yanga bado wapo kwenye mazungumzo na beki Andrew Vincent ambaye mkataba wake pia umeshamalizika.

Beki huyo anaaweza akamwaga wino wa mwaka mmoja pia kuungana na wenzake tajwa hapo juu tayari kukipiga msimu ujao.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic