July 12, 2018


Klabu ya Singida United imefanikiwa kuinasa saini ya  mchezaji Feisal Salum Abdalah “FEI TOTO” kwa kandarasi ya miaka mitatu.

Katika kikao cha pamoja cha Uongozi wa JKU na Singida United, wameshakubaliana gharama za kufidia mkataba (transfer fee) wa miaka miwili ambayo mchezaji huyo alibakiza kuitumikia JKU.

Toto ambaye alikuwa akihusishwa kutua Yanga amefikia makubaliano na uongozi wa Singida kwa kusaini kandarasi hiyo na sasa atakuwa sehemu ya kikosi cha walima alizeti hao katika msimu ujao wa Ligi Kuu Bara.

Hii ni mwendelezo wa kukisuka kikosi cha SU chini ya kocha Hemedi Selemani Morocco.

3 COMMENTS:

  1. Hivi kumbe sio Simba tu wanaoiba wachezazi ambao Yanga wamekuwa wanafikiria kuwasaji.Singida na Azam nao wamo.

    ReplyDelete
  2. Mchezaji ana maamuzi yake. Siyo kwamba wanawaiba. Na ujue Yanga ni timu kubwa ili habari ya huyu jamaa anatunga habari za uongo zipate soko lazima aandike hapo Yanga. Pengine hata Yanga hawajawahi kumfikiria kijana. Yanga taifa kubwa. Itashangaza ulimwengu msimu ujao. Endeleeni kuibeza tu.

    ReplyDelete
    Replies
    1. weweeee unasemaje? Yanga haijawahi kumfikiria? Haya sasa breaking news ... Yanga wamemsajili mtoto huyo kutoka JKU kutoka Singida United. Yanga hiyooooo sera ya kimya kimya

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic