RONALDO NA HIGUAIN, YAYA TOURE NA WEST HAM: TETESI ZA SOKA ULAYA LEO ALHAMIS
West Ham wameanzisha mazungumzo na aliyekuwa kiungo wa kati wa Manchester City Yaya Toure, lakini wanadaiwa kusita kumpatia kandarasi mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 35 . (Sun)
Baada ya kumsaini Cristiano Ronaldo, Juventus wanatarajiwa kumuorodhesha mshambuliaji wa Argentina Gonzalo Higuain, 30, ambaye anahusishwa na uhamisho wa Chelsea kuwa miongoni mwa wanaotarajiwa kuuzwa msimu huu.(Calciomercato)
Chelsea wanapigiwa upatu kumsaini kiungo wa kati wa Napoli na Itali Jorginho, 26. (London Evening Standard)
Croatia walivyosherehekea kuwashinda England, London masikitiko tu
Manchester City wanaamini kwamba Jorginho hatahivyo anataka kujiunga nao.(Manchester Evening News)
Everton wanajaribu kushinikiza kumnunua beki wa Barcelona na Colombia Yerry Mina, 21, kwa dau la £21m (Mirror)
Mchezaji anayelengwa na Liverpool Nabil Fekir, 24, ameiambia Lyon kwamba bado anataka kuelekea Anfield , huku mshambuliaji huyo wa Ufaransa akizitaka klabu hizo mbili kufufua mazungumzo baada ya fainali ya kombe la dunia. (Mirror)
Liverpool inakabiliwa na ushindani mkali katika kumzuia kinda wa Uingereza Rhian Brewster, 18, baada ya mshambuliaji huyo kuvutia klabu za PSG na Juventus huku naye akiendelea kuchelewesha mkataba mpya na klabu hiyo ya Anfield. (Sun)
Mmiliki mwenza wa klabu ya West Ham David Sullivan anasema kuwa klabu hiyo iko tayari kuongeza wachezaji wengine baada ya kusajili watano huku wakiendelea kuzungumza na kiungo wa kati wa Lazio na Brazil Felipe Anderson, 25. (Sky Sports)
Cardiff inakaribia kumsajili tena kiungo wa kati wa Liverpool na Serbia Marko Grujic, 22, kwa mkopo. (Football Insider)
West Brom ina hamu ya kumsajili mshambuliaji Kemar Roofe, 25, kutoka Leeds. (Birmingham Mail)
Juventus inafuatilia usajili wa Cristiano Ronaldo na mpango wa kumsajili beki wa Uruguay na Atletico Madrid Diego Godin, 32. (Tuttosport via Sun)
Mabingwa hao wa Itali pia wamefanya mazungumzo na wawakilishi wa Matteo Darmian huku wakitaka kumsaini beki huyo wa kushoto wa Manchester United kwa dau la £17m. (Talksport)
Kinda wa Nottingham Forest Matthew Bondswell amekataa maombi ya Manchester United na Liverpool ili kujiunga na klabu ya RB Leipzig. (Sun)
Barcelona inajiandaa kuanza mazungumzo na kiungo wa kati wa PSG Adrien Rabiot, 23, ambaye hakuorodheshwa katika kikosi cha kombe la dunia cha Ufaransa . (Mundo Deportivo - in Spanish)
Kutoka BBC
0 COMMENTS:
Post a Comment