July 12, 2018


Imeripotiwa kuwa uongozi wa klabu ya Kiyovu kutoka Rwanda umetishia kwenda FIFA kwa madai ya mchezaji wake, Fabrice Kakule, kuonekana na timu ya Simba akifanya mazoezi jijini Dar es Salaam.

Taarifa kutoka Rwanda zinaeleza kwa mujibu wa Rais wa Kiyovu, Jean Pierre, amesema atafanya mipango ya kupeleka mashtaka FIFA akieleza kuwa Kakule bado ana mkataba na Kiyovu ambao unamaliza mwaka kesho.

Pierre amefunguka akiwataka Simba ni vema wakakutana kufanya makubaliano juu ya mchezaji wake badala ya kumsajili kinyemela, jambo ambalo linaenda kinyume na tataribu za usajili wake.

Inaelezwa kuwa Kakule atakuwa anamaliza mkataba wake mwishoni mwa mwezi Julai mwaka kesho hivyo Pierre amewataka Simba kumuachia mchezaji wake mara moja au wakae mezani ili waweze kumalizana.

Kakule tangu awasili nchini amekuwa akifanya mazoezi na mabingwa hao wa Ligi Kuu Bara msimu wa 2017/18 ambacho kipo katika mashindano ya KAGAME yanayoendelea hivi sasa jijini Dar es Salaam.


3 COMMENTS:

  1. Atangulie tu FIFA nasisi tuna kesi yetu ya Ubingwa huko tunaifuatilia tutakutana hukohuko.

    ReplyDelete
  2. Jamani chama langu la msimbazi vipi tena? Nasikia huyu mkongomani bado ana mkataba unaoisha mwakani mwezi wa 7. Timu yake anayoichezea sasa hivi Kiyovu Sports ya Rwanda inataka kuipeleka Simba Fifa kuilalamikia kufanya mazungumzo na kumfanyisha mazoezi mchezaji wao ambaye bado ana mkataba....Jamani ehe pamoja na kwamba tuna shida ya wachezaji wa kigeni lakini tufanyeni mambo kwa weledi kidogo tusije kuingia kwenye matatizo, na hizi pesa za mwekezaji zitumiwe vizuri sio kwa pupa. Haya mambo kama ni kweli basi Simba tutaumia kweli na mkono wa Fifa

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic