July 10, 2018


Nahodha wa klabu ya Yanga, Nadir Haroub 'Cannavaro', amekiri kuwa klabu yao inapitia wakati mgumu hivi sasa na akiamini siku za usoni itarejea kuwa kama zamani.

Cannavaro ambaye hakucheza mechi nyingi za takribani msimu mzima wa ligi uliopita, ameeleza kuwa viongozi wake wanapambana kumaliza matatizo yaliyopo hivi sasa.

Beki huyo aliyeichezea Yanga kwa mafanikio makubwa anaamini klabu imeyumba kifedha kutokana na wakati inaopitia japo akipiga moyo konde kuwa ile furaha ya zamani itarudi hapo baadaye.

Wakati Yanga ikipitia hali hiyo, kikosi cha timu hiyo kipo katika maandalizi ya mashindano ya Kombe la Shirikisho Afrika ambapo Julai 18 watakuwa wanacheza dhidi ya Gor Mahia FC ya Kenya.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic