July 9, 2018
 Kiungo Hassan Dilunga anayewaniwa na mabingwa wa Tanzania Bara, ametangazwa kuwa mchezaji bora wa msimu  wa 2017/18 katika kikosi cha Mtibwa Sugar.

Dilunga ametangazwa kuwa mchezaji bora na kupewa tuzo na mkwanja wake 'live'.

Kiungo huyo aliyewahi kucheza Yanga alikabidhiwa tuzo yake wakati wa sherehe ya tuzo za Mtibwa Sugar zilizofanyika kwenye Hoteli ya New Afrika jijini Dar es Salaam, jana.

Dilunga amekuwa akiwaniwa na Simba na tayari imeelezwa Mtibwa Sugar iko tayari kumuachia kama mabingwa hao "watawapa chao".

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV