July 9, 2018





 Beki wa Mtibwa Sugar, Hassan Isihaka ametangazwa kuwa mchezaji mwenye nidhamu ya juu zaidi katika kikosi chake kwa msimu wa 2017/18.

Isihaka ambaye aliwahi kucheza Simba, ameteuliwa kuwa mchezaji mwenye nidhamu zaidi katika kikosi cha Mtibwa Sugar na kupewa tuzo.

Beki huyo wa kati alikabidhiwa tuzo na “bahasha” yake wakati wa sherehe ya tuzo za Mtibwa Sugar zilizofanyika kwenye Hoteli ya New Afrika jijini Dar es Salaam, jana.

Mtibwa Sugar ilitoa tuzo kwa wachezaji wake mbalimbali na tutaendelea kukuletea.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic