July 10, 2018


Na George Mganga

Uongozi wa klabu ya Yanga umemsajili kiungo mshambuliaji wa Mtibwa Sugar, Mohammed Issa Banka kwa kusaini naye mkataba wa miaka miwili.

Kiungo huyo anaungana na Yanga iliyo kwenye maandalizi ya michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika ambapo ipo kambini hivi sasa.

Usajili huo umekamilika ikiwa ni siku kadhaa zimepita baada ya kuwaongezea mikataba wachezaji wake, kipa Beno Kakolanya na beki wa kulia Juma Abdul pamoja na kumrejesha aliyekuwa kiungo wake, Deus Kaseke kutoka Singida united.

Yanga inaendelea kujifua kuelekea mchezo dhidi ya Gor Mahia utakaokuwa wa mkondo wa kwanza huko jijini Nairobi Kenya.


2 COMMENTS:

  1. Imekuwaje tena mbona walisema wao hawatangazi usajili wao. Hiyo ndiyo kimya Kimya?

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic