Usidhani kwamba Bilionea, Yusuf Manji hajui kinachoendelea Simba. Anamjua mpaka Mbelgiji, Patrick Aussems aliyeko Dar es Salaam kwa mazungumzo na muwekezaji Mohammed Dewji ‘MO’.
Manji huenda akatoa tamko la kurudi Yanga muda wowote kuanzia sasa baada ya kuwasikiliza viongozi wa timu hiyo ambayo wanachama wote wameafiki aombwe arudi ingawa inadaiwa huenda akaja na masharti mengi.
Mmoja wa viongozi wa Yanga inayobezwa na baadhi ya mashabiki kwa kumrejesha kundini Mrisho Ngassa, aliiambia Spoti Xtra jana kwamba Manji anayeishi kilomita chache kutoka katikati ya Jiji la Dar es Salaam, anajua kila kinachoendelea kwenye michezo na anafuatilia kabla hajaamua kurudi rasmi Jangwani.
“Anajua kila kitu kinachoendelea, hata stori za kocha mpya aliyekuja Simba anazijua,alipata siku ileile,” alidokeza kiongozi huyo mwenye ushawishi mkubwa ndani ya Yanga iliyojitoa kwenye michuano ya Kagame.
Alisema kwamba dalili za Manji kurejea Yanga iliyoko chini ya udhamini mkuu wa SportPesa ni kubwa ndio maana ameanza kufuatilia kila kinachoendelea kwa ukaribu na huwezi kumdanganya chochote.
Mwenyekiti huyo ambaye ni mwanachama wa CCM, aliyejiuzulu Yanga mwaka mmoja uliopita, amewaambia viongozi wa Yanga kwamba wampe muda kidogo afya yake ikae sawa na vilevile apate muda wa kujadiliana na familia yake.
Lakini habari za uhakika zinasema kwamba mbali na viongozi wa Yanga vilevile amefuatwa na watu wakubwa serikalini wakimshawishi kurejea Yanga ingawa amewaambia baadhi kwamba anafikiria kurejea kama mshauri na mwanachama wa kawaida.
Yanga ambayo msimu uliopita ilitema ubingwa wake, inajiandaa na mechi ya makundi ya Shirikisho dhidi ya Gormahia ya Kenya Julai 18 jijini Nairobi.
CHANZO: SPOTI XTRA
Mbona kwenye habari nzima sijaona kifungu chochote kinachoelezea ni jinsi gani Manji anamjua huyo M-belgiji wa Simba!!!!!
ReplyDeleteMbona mwandishi wa hii blog anatufanya sisi wasomaji wajinga sana,yaani anatuchukulia kama mazumbukuku tusio na uelewa wowote!!!
Acha kuuza habari kijinga. Kama anamfahamu nn point yako hapo. Hadi unaboa kaka.
ReplyDeleteThis comment has been removed by the author.
ReplyDeleteHuko ndo kumjua kocha au njaa tu na we
ReplyDeleteHuu ni upuuzi
ReplyDeleteFanya blog ya mapenzi, ili Uwe guru kuandika mawazo yako hata yakiwa ya uongo
ReplyDelete