July 9, 2018


Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Clement Sanga, ameweka wazi kuhusiana na mrejesho wa aliyekuwa Mwenyekiti wao Yusuf Manji ambaye ombi lake la kuomba kujiuzulu lilipingwa na wanachama kuwa amekubali kurejea, imeelezwa.

Katika mkutano mkuu wa klabu uliofanyika Juni 10 kwenye ukumbi wa Bwalo la Polisi, Oysterbay jijini Dar es Salaam, idadi kubwa ya wanachama ilipinga barua hiyo na kuazimiwa wote kuwa inabidi aendelee kuwa Mwenyekiti.

Sanga ambaye amekaimu nafasi ya Manji, amefunguka na kusema kuwa wamejitahidi kufikisha kauli hiyo ya wanachama wa Yanga na akaeleza kuwa Mwenyekiti amekubali kurejea japo atahitaji muda kidogo.

Kwa mujibu wa Sanga aliyekuwa na viongozi wa matawi katika kikao, amesema hayo kuwa wameshafikisha taarifa hiyo kwa Manji na kuna uwezekano mkubwa akarudi kwa kishindi siku chache zijazo.

Wakati Yanga wakiendelea na jitihada za kumshawishi Manji arudi, timu ipo kambini hivi sasa ikijiandaa na mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Gor Mahia Fc utakaopigwa Julai 18 jijini Nairobi.

7 COMMENTS:

  1. Mkuu siku hizi umeanza kuandika habari za michezo kama udaku..! Unachokisoma ndani hakiendani na kichwa cha habari husika...na mbaya zaidi habari nyingi hazieleweki.

    ReplyDelete
  2. Sasa hii ni Historia au Habari? Mbona haisemi kikao kikekaa lini na wapi juu ya ajenda ya Manji?

    ReplyDelete
  3. This comment has been removed by the author.

    ReplyDelete
  4. This comment has been removed by the author.

    ReplyDelete
  5. This comment has been removed by the author.

    ReplyDelete
  6. Manji amesema baada ya miezi 3, wakati klabu itakuwa imeshajifia....timu haiwezi kukaa bila ya uongozi wa mwenyekiti kwa kipindi hicho chote....hakuna dira, mwelekeo, na ufanisi, VIONGOZI wakiongozwa na Sanga wote wamekuwa wababaishaji, waongo, wakipiga njama za kuitafuna pesa ya CAF. Wachezaji wanadai mishahara, usajili wa kuunga unga, na 10% wanawafanya wanachama na wapenzi wa Yanga kama watoto na wajinga. Mkutano uliofanyika mwezi uliopita ulishaunda kamati ya mpito lakini figisu zimerudi tena tofauti na watu walivyotegemea!

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic